AWARDS PRESENTING CEREMONY FOR THE DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2014
0
Afisa mtendaji mkuu wa Dar es Salaam Stock Exchange akiongea
na wanafunzi walioshiriki katika shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment
Challenge 2014” wakati wa hafla ya kuwatambua wanafunzi hamsini bora na
uandaaji wa mchakato wa kutafuta washindi watatu bora wa shindano hilo.
Katikati ni bwana George Kivaria mwakilishi benki ya NMB (wadhamini wa
mashindano) kushoto ni Sosthenes Kewe Mkurugenzi
wa taasisi ya uendelezaji wa huduma za fedha.
Baadhi ya wanafunzi hamsini bora wakikabidhiwa vyeti vyao
na wageni rasmi, wa kwanza kotoka kushoto ni George Kivaria mkuu wa kitengo
cha huduma mbadala Benki ya NMB, wapili Sosthenes
Kewe Mtendaji mkuu taasisi ya
uendelezaji wa huduma za fedha.
Wanafunzi wa vyuoni wakijiandaa kujibu maswali (kuhojiwa) katika
mchakato wa kumtafuta mshindi wa shindano la uzekezaji “DSE Scholar Investment
Challenge 2014”
Majaji wakifatilia majibu ya wanafunzi jinsi namna
walivyofanya maamuzi ya uwekezaji katika shindano la uwekezakaji “DSE Scholar
Investment Challenge”
wadau wa soko wa soko la hisa la Dar es Salam “Dar es Salaam Stock Exchange”
wakifuatilia mchakato wa kutafuta washindi watatu bora.
Mshindi wakwanza wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar
Investment Challenge 2014” Laurent Dyanko kutoka chou kikuu cha kilimo, Sokoine
University of Agriculture (SUA) akikabidhiwa zawadi wa shilingi milioni moja na
cheti cha ushindi.
Laurent Dyanko aliweza kutumia mtaji wa milioni moja (mtaji
aliogewa baada ya kujisajili katika mashindano) na kuwekeza Soko la hisa la Dar
es Salaam na kuweza kuuongeza thamani kufikia takribani shilingi milioni nne na
laki moja ndani ya mienzi minne.
Mshindi wapili wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar
Investment Challenge 2014” George Firimini kutoka chuo cha usimaniza wa fedha, Institute
of Finance Management (IFM) akikabidhiwa zawadi wa shilingi laki sita na cheti
cha ushindi
Mshindi watatu wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar
Investment Challenge 2014” Godlove Kellya kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam
akikabidhiwa zawadi ya shilingi laki nne na cheti cha ushindi